RISK/REWARD RATIO KATIKA KU TAKE PROFIT & STOP-LOSSđĽ
Katika biashara ya sarafu za kidijitali (crypto trading), âRisk/Reward Ratioâ inamaanisha kiasi unachokubali kuhatarisha katika biashara ikilinganishwa na faida unayolenga kuipata.
Mfano:
âRisk/Reward Ratio: Lenga 3:1 ili kuongeza faida,â inamaanisha:
1. Kwa kila dola 1 unayohatarisha, lengwa lako ni kupata dola 3 kama faida.
2. Kwa mfano, kama uko tayari kupoteza dola 100 (stop-loss), basi unapaswa kulenga kupata dola 300 (take-profit).
Kwa nini uwiano wa 3:1 ni mzuri?
1. Hata kama utashinda biashara 1 kati ya 3, bado hutapoteza mtaji wako.
2. Ukishinda zaidi ya 1 kati ya 3, utakuwa unapata faida kwa muda mrefu.
Mfano:
Unaingia ku trade Bitcoin:
1. Bei ya kuingia: $50,000
2. Stop-loss: $49,500 (unahatarisha $500)
3.Take-profit: $51,500 (unalenga $1,500)
Huu ni uwiano wa 3:1, kwa sababu unahatarisha $500 ili kupata $1,500.
Ni kanuni ya usimamizi wa hatari ambayo huwasaidia wafanyabiashara kulinda mtaji wao na kuongeza faida kwa muda mrefu.