😳😢WATANZANIA HUTUMIA 1% YA AKILI ZAO: [MWAKA 2023 GAZETI HILI LILIANDIKA]📈

2 HABARI

Watanzania hutumia asilimia moja ya akili zao

NA NEEMA NIVAMAMBA

IMEELEZWA kuwa asilimia kubwa ya Watanzania hutumia asilimia moja tu ya akili zao katika maisha ya kila siku.

Rai hiyo imetolewa jana Mkurugenzi wa Taasisi ya Maji na Mazingira Mkoani Morogoro, Mussa Maganga alipokuwa akitoa elimu ya mazingira kwa kikundi cha vijana, wanafunzi na wananchi wa kata ya Kihonda katika stendi ya Waislamu mjini hapa kuhusu matumizi ya akili katika maisha ya kila siku.

Alisema binadamu wengi hawatumii akili zao kikamilifu kwa sababu ya kushindwa kupanga vizuri maisha yao na kutumia muda mwingi katika kufanya mambo yasiyo ya msingi hali inayosababisha kushindwa kufikia malengo waliyojiwekea.

Pia alisema binadamu ana hali kubwa sana ya uwezo wa kufikiri lakini wengi hushindwa kuitumia hali hiyo katika maisha yao ya kila siku hali inayosababisha kukumbwa na matatizo mbalimbali.

Kauli hiyo aliitoa wakati akizungumza na vijana katika maonesho ya mazingira yaliyofanyika kuanzia Septemba 22 na 23 mwaka huu, yaliyofanyika stendi ya Waislamu, Kihonda mjini hapa yakihusisha kikundi cha vijana kutoka maeneo mbalimbali.

Hata hivyo Maganga alibainisha kuwa moja ya sababu kubwa ya hali hiyo ni mtindo wa maisha Kipuuzi kwa baadhi ya Watanzania ambao hushindwa kutumia muda wao kwa mipango endelevu katika maisha yao.

Alisema katika maonesho hayo zaidi ya vijana 1,300 walitembelea banda la taasisi hiyo wakitoka katika Wilaya sita ikiwemo, Kilombero, Ulanga na Temeke.

Anza Safari Yako Ya Sarafu Mtandao